John 1

Neno Alifanyika Mwili

1 aHapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 bTangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.

3 cVitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4 dNdani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 eNuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda.

6 fAlikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7 gAlikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini. 8 hYeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 9 iKwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni.

10 jHuyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. 11 kAlikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 12 lBali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13 mHawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.

14 nNeno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.

15 oYohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ” 16 pKutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 qKwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)

19 rHuu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20 sYohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


21 uWakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

23 vAkawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25 wwakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”

26 xYohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,
Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji.
lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua.
27 zYeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”

28 aaMambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.

Yesu Mwana-Kondoo Wa Mungu

29 abSiku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 acHuyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 31 adMimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”

32 aeKisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 afMimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 agMimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”

Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu

35 ahSiku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 aiAlipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!”

37Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38 ajYesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”

Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?”

39Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”

Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

40 akAndrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu. 41 alKitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 42 amNaye akamleta kwa Yesu.

Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro
Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake ni Kipande cha mwamba.
).

Yesu Awaita Filipo Na Nathanaeli

43 aoSiku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

44 apBasi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 45 aqFilipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.”

46 arNathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”

47 asYesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.”

48Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?”

Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”

49 atNathanaeli akamwambia, “Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”

50Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 51 auNdipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

Copyright information for SwhNEN